Ø Hupunguza athari
za kiuchumi zitokanazo na maambukizi.
Ø Hulinda afya za
kuku ambao hawajaambukizwa.
Ø Hupunguza kuenea
kwa maambukizi kutoka kuku wagonjwa kwenda kuku wasio wagonjwa.
Ø Huwakinga
wanadamu wasipate maambukizi kutoka kwa kuku wagonjwa.
Ø Huzalisha kuku
na bidhaa zenye ubora wa juu ambazo hupata bei nzuri sokoni.
UTEKELEZAJI
WA TARATIBU ZA KUZUIA KUENEA KWA MAGONJWA
Taratibu za Kuzuia Kuenea kwa Magonjwa
hutekelezwa kwa lengo la kuzuia uingiaji na usambaaji wa vimelea vya ugonjwa
ndani na kati ya vijiji, kaya na mashamba. Taratibu hizi ni pamoja na kuweka
karantini ambapo magonjwa na vimelea vya ugonjwa huzuiwa kuingia katika eneo
fulani, au vimelea huharibiwa na kuzuiwa sehemu moja ili
visipenye kuingia
maeneo mengine. Hivyo basi, taratibu za kuzuia kuenea kwa magonjwa zina
vipengele vikuu vitatu: karantini, kudhibiti njia za usafirishaji na usafi wa
maeneo.
Programu imara ya
kuzuia kuenea magonjwa ni muhimu sana ili uweze kuendelea kuwa na kuku wenye
afya. Unapotayarisha programu hii katika shamba la kuku, vipengele vitatu vya
kuzingatia ni:
1.
Eneo lilipo shamba au banda: Shamba au banda la kuku liwe
mbali na mashamba mengine ya ndege na mifugo mingine. Ni vyema banda moja
likawa na kuku wa umri mmoja ili kuzuia vimelea vya magonjwa
kuendelea kubaki
bandani.
2.
Ramani ya shamba au banda: Kujenga uzio ili kuzuia watu
wasiohusika kuingia shambani au bandani. Mchoro wa mabanda upunguze pita pita
za watu na uwezeshe usafi na upuliziaji wa dawa kufanyika kwa urahisi. Jenga
mabanda yenye nyavu ambayo ndege pori na panya hawawezi kuingia.
3.
Taratibu za kuendesha shughuli za shamba: Zuia kuingizwa na
kuenezwa kwa magonjwa shambani
kwa kudhibiti
uingiaji wa watu, vyakula, vifaa, wanyama na magari ndani ya shamba.
Hatua za
Tahadhari za Kuzuia Kuingia na Kuenea kwa Magonjwa Shambani
Ø Tenganisha
ndege kufuatana na aina ya ndege na umri wao
Ø Weka
karantini kwa ndege/kuku wapya ili wachunguzwe kwa kipindi kisichopungua wiki
mbili
kabla ya kuingizwa
shambani au bandani.
Ø
Usiruhusu tabia ya kuchangia vifaa/vyombo kama vile makasha ya
mayai, makreti ya kubebea kuku
kati ya shamba na
shamba, n.k.
Ø
Wafanyakazi waanze kuwahudumia kuku wenye umri mdogo kabla ya wale
wenye umri mkubwa.
Ø Usiruhusu
watoto kucheza na kuku.
Ø Jaribu
kuzuia idadi ya wageni wanaoingia shambani/bandani.
Ø Weka
utaratibu wa kuangamiza mizoga ya kuku.
Ø Anzisha
programu jumuishi ya kudhibiti wadudu/wanyama waharibifu.
Ø Panga
utaratibu mzuri wa kuwapa kuku huduma ya maji na kufanya usafi.
Ø Panga
utaratibu mzuri wa kuzoa taka na mizoga ya kuku.
Ø Panga
utaratibu mzuri wa kusafisha banda na kupulizia dawa.
Ø Vifaa
visafishwe na kuwekwa dawa ya kuua vijidudu kabla ya kuingizwa shambani.
Ø Hakikisha
magari yanapoingia shambani yanapita katika kidimbwi chenye dawa ya kuua vimelea
vya magonjwa.
Ø
Hakikisha mfanyakazi anabadilisha viatu/mabuti kabla ya kuingia
katika kila banda
Ø
Weka taratibu nzuri za kuingia shambani, ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha usafi wa viatu na mikono; au wageni na wafanyakazi kubadilisha
nguo/viatu na kuvaa mabuti.
MAGONJWA MUHIMU YA
KUKU/NDEGE WAFUGWAO
Ugonjwa
ni nini? Ugonjwa ni mabadiliko kutoka katika afya ya kawaida ya
mnyama/kuku. Hali hii hutokea pale
vimelea au vijidudu
vinapoingia mwili wa mnyama, kwa kula vyakula vyenye sumu, au inapotokea kuna
uhaba wa lishe au madini mwilini.
TOFAUTI
ZA MUONEKANO KATI YA KUKU MWENYE AFYA NA KUKU MGONJWA
KUKU
MWENYE AFYA NZURI
Ø Macho
na sura angavu
Ø Hupenda
kula na kunywa maji
Ø Pua
zilizo safi, upanga na undu mwekundu, manyoya
laini na yaliyopangika vizuri
Ø Hupumua
kwa utulivu
Ø Sehemu
ya kutolea haja huwa kavu
Ø Kinyesi
kikavu, cheupe na kisicho na rangi
Ø Hutaga
mayai kawaida
KUKU ASIYE NA AFYA NZURI
Ø Huonekana
mchovu na dhaifu
Ø Hula
na kunywa kidogo au zaidi ya kawaida
Ø Hutoa
kamasi puani, ute na matongotongo; manyoya
yaliyovurugika
Ø Hupumua
kwa shida na kwa sauti
Ø Sehemu
ya kutolea haja inakuwa na unyevunyevu na
kinyesi kuganda
Ø Huharisha,
kinyesi huwa na damu au minyoo
Ø Hutaga
mayai machache au husimama kutaga kabisa
Ø Huwa
na tabia ya kujitenga na wenzake katika kundi